WATU 15 wamekufa katika ajali iliyohusisha lori lililogonga magari kadhaa katika jimbo la Alexandria nchini Misri, mamlaka imesema.
Ajali hiyo iliyotokea Jumanne jioni katika Wilaya ya Amreya, Magharibi mwa mji wa Alexandria, pia ilijeruhi watu wanane.
Lori hilo liligonga mabasi manne madogo na gari dogo la abiria ambalo, ripoti hiyo ilisema. Ilisema basi moja lilipinduka na la pili likawaka moto.
Ambulensi ziliwahi eneo la ajali na kuwasafirisha watu waliojeruhiwa hadi hospitali, kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani.