Akiba fedha za kigeni dola mil. 5,345.5

DODOMA : WAZIRI wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba  amezungumzia hali ya akiba ya fedha za kigeni iliyokuwepo nchini ambapo kwa sasa akiba ya fedha za kigeni imefikia dola za kimarekani milioni 5,345.5 ukilinganisha na mwaka 2023 ilikuwa dola milioni 5,446.1.

Akiwasilisha mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/2025 bungeni mjini Dodoma,  Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba  amesema katika kipindi cha miezi minne serikali imetumia akiba ya fedha za kigeni kuagiza bidhaa na huduma zingine kutoka nje ya nchi.

Akizungumzia kuhusu akiba ya dhahabu iliyokuwepo katika Benki Kuu ya Tanzania- BOT,Dk. Mwigulu amesema akiba ya dhahabu imefikia kilo 976.51, yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 89.96 sawa na asilimia 16.3 ya lengo la makusanyo ya kilo 6000 kwa mwaka 2024/25.

Advertisement

kuhusu akiba ya chakula, Dk. Mwigulu amesema katika ghala la Taifa kwa hifadhi ya NFRA kulikuwa na tani 826,000 ambapo uzalishaji ulikuwa tani milioni 22, sawa na asilimia 128% ambapo lengo la nchi ni kufikia tani 130 mwaka 2025/26.

“ Hii ni serikali inayotenda kwa vitendo, na  haijawahi kutokea”, Alisema  Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba.

SOMA :Dk Mwigulu awasilisha mapendekezo ya Sh trilioni 43.3 bajeti 2023/24