Akili ya Arsenal bado ipo kwa Benjamin Sesko

KWA mujibu wa tetesi za usajili Arsenal-The Gunners, inaendelea kufuatilia maendeleo ya mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia, Benjamin Sesko, ambaye alikuwa mlengwa wa usajili wa The Gunners wakati wa dirisha la uhamisho majira ya kiangazi. (football.london)

Manchester United inapewa kipaumbele hatimaye kumsajili kiungo wa kidachi Frenkie de Jong iwapo ataondoka Barcelona majira yajayo ya kiangazi. (Fichajes – Spain)

Manchester City inataka kumpatia Erling Haaland mkataba mpya na kubadilisha vifungu vya kuachiliwa vinavyomruhusu kuondoka kwenye klabu katika siku zijazo.(TBR Football)

SOMA: Arsenal yaitangulia Juve kuwania saini ya Calafiori

Liverpool ipo katika hatua ya mbele ya mazungumzo kupata saini ya beki wa kati wa Sevilla, Loic Bade wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2025. (Fichajes – Spain)

Barcelona inataka kusajili golikipa mpya wa kiwango cha juu kuziba nafasi ya Marc-Andre ter Stegen na inaona Diogo Costa wa Porto anafaa kuwa lengo lake namba moja. (El Nacional – Spain)

Pia klabu hiyo imeonesha nia kwa Joan Garcia wa Espanyol na David Raya wa Arsenal. (El Nacional – Spain)

Mivutano inayoongezeka kati ya Chelsea, Liverpool na Manchester United imesababisha maskauti kuzuiwa kuingia kwenye mechi za timu za vijana. (The Athletic)

Kiungo wa Bayern Munich, Joshua Kimmich bado anawaniwa na Manchester City, Liverpool na Barcelona, lakini miamba hiyo ya Bavaria ina tumaini atasaini mkataba mpya. (HITC)

Habari Zifananazo

Back to top button