ZAIDI ya wanafunzi 300 wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia cha AL-MAKTOUM wamefanya ubunifu wa mifumo mbalimbali ili kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Hayo yamesemwa katika mahafali ya 11 leo jijini Dar es Salaam na mkuu wa chuo hicho, Dk Hamdun Sulayman ambapo wanafunzi 82 waliihitumu kozi mbalimbali.
Dk Hamdun amesema tangu mwaka 2010 hadi 2023 jumla ya wanafunzi 723 walihitimu ambapo wasichana ni 86 huku wavulana wakiwa ni 637.
“Kwa siku ya leo wanaohitimu ni wanafunzi 82 kati yao wasichana ni wanane na wavulana ni 74 kwa idadi ya muhitimu wapo waliojiajiri na kutoa ajira kwa wanachi na wapo wanaopata elimu nje ya Tanzania,”ameeleza.
Amesema Chuo kinakuza bunifu kwa vijana kwa ajili ya kutatua changamoto ambapo walibuni malipo ya mfumo wa maji na kuisaidia jamii.
“Elimu ya mafunzo tunayotoa ni ya kiwango cha juu tunaamini wahitimu wetu ni wazuri tunaamini wataleta suluhu katika jamii na kuleta mchango mkubwa na pia tunathamini mchango mkubwa wa serikali na wadau.
Ameaisha changamoto zilizopo kuwa ni idadi ndogo ya udahili ya wanafunzi wakati wanauwezo wa kufundisha wanafunzi 700 ila mara nyingi wanapokea 250.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -Tamisemi, Adolf Nduguru amewataka wanafunzi hao watumie walichojifunza kuleta mabadiliko katika jamii zao.
” Wasibweteke watumia fursa kujiajiri na kuendeleza miradi waliyoanzisha na pia wajiendeleze na kufikia ubobevu mkawe tayari kujifunza huko mnakokwenda teknolojia inabadili kila siku hivyo muendane nayo,”amesisitiza.
Ameongeza “Wahitimu nendeni mkawe mabalozi wema wa kutangaza chuo hiki watu wajue ili vijana zaidi waje
tunaendelea kuboresha ujifunzaji wa masomo ya sayansi na teknolojia wanafunzi watapatikana.
Naye Mkurugenzi wa bodi ya chuo hicho Prof Hamisi Omar amesema matarajio yao ni kuweza kuendesha chuo kifedha hivyo ni lazima watafute utaratibu.
“Tumeweka mitaala mipya hivi karibuni na taasisi ya teknolojia inakua haraka ulimwenguni na mambo yanabadilika kama akili bandi tunahakikisha yanayofanyika yanafanyika kikamilifu hatuwezi kuIipa kisogo.
Radhia Nassor ambaye ni mhitimi wa mhandisi wa umeme amesema miongoni mwa mradi aliofanya ni kuhusu udongo akiangalia unyevu na joto.
“Tatizo lilikuwa wakulima hawapati taarifa muhimu ya kilimo bora napima katika udogo kuangalia ni aina gani ya mazao yanahitaji tunaangalia kiwango cha maji na utofauti ni progarmu yetu inatoa taarifa kupitia simu.