Alexander Isak azikataa Man United, Arsenal
TETESI za usajili zinasema mshambuliaji wa Newcastle United, Alexander Isak, zmezikataa Manchester United na Arsenal huku mchezaji huyo machachari akiependelea kujiunga na Barcelona. (El Nacional – Spain)
Bayern Munich inakusudia kuendelea kuadiliana mkataba mpaya na Joshua Kimmich licha ya kuondoa ofa yake ya hivi karibuni. (Sky Germany)
Arsenal ipo katika harakati za kukamilisha kumsajili Kimmich kabla ya Barcelona na inamchukulia mjerumani huyo kama kipaumbele chake. (El Nacional – Spain)
Manchester City ina nia kumsajili kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, Michael Olise huku kocha wa City Pep Guardiola akiwa na imani nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kutua Etihad. (Fichajes – Spain)
Liverpool inaendelea kuonesha nia kumsajili nyota mwenye uwezi wa kucheza nafasi nyingi wa Ajax, beki Jorrel Hato, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 40, na pia majogoo hao wanawakodolea macho Anton Gaaei na Mika Godts. (TBR Football)



