HAITI : BARAZA la Mpito nchini Haiti limemchagua Alix Didier Fils- Aime kuwa Waziri Mkuu mpya nchini humo.
Uamuzi huu umekuja baada ya Baraza hilo kusaini amri ya kumfukuza Waziri Mkuu Mpito Garry Conille ambaye alishika nafasi hiyo kwa muda.
Wabobezi wa masuala ya siasa nchini humo wamesema uamuzi huo wa kumfukuza kazi Connille kunaweza kuleta mivutano ya kisiasa hasa katika kipindi cha kusimamia mchakato wa demokrasia nchini humo.
Baraza hilo liliteuliwa mwezi Aprili na kupewa jukumu la kumchagua waziri mkuu na baraza la mawaziri ambalo wanaamini linaweza kusaidia kutuliza mzozo nchini Haiti.
Hata hivyo baraza hilo limekumbwa na mivutano ya kisiasa kwa baadhi ya wajumbe ambao wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi. SOMA: