Aliyekuwa mkurugenzi jela miaka 20 uhujumu uchumi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imewahukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima na wenzake wawili kifungo cha miaka 20 jela baada ya kukutwa na makosa ya uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Agosti 31, 2023 na Hakimu Seraphin Nsana katika kesi namba 5/2022 ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili Dk Pima akiwa na wenzake aliyekuwa muweka hazina wa jiji la Arusha Mariam Mshana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji, Innocent Maduhu.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5/2022, mbele ya mahakama, Hakimu Seraphin Nsana alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili mahakama imewatia hatiani washtakiwa katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inawakabili.

Advertisement

“Kwa kuzingatia maombi ya mawakili wa upande wa washtakiwa, ikiwemo kutokuwa na rekodi ya makosa ya nyuma, utegemezi wa familia na ushirikiano mlioutoa katika kipindi chote cha uendeshaji wa kesi hii, mahakama inawapa adhabu ya kutumikia miaka 20 jela huku miezi 14 mliokuwa kizuizini ukizingatiwa”

Mbali na hilo, washtakiwa wamepewa nafasi ya kukata rufaa katika mahakama  kuu endapo hawajaridhika na jukumu hiyo

Awali baada ya kutiwa haitiani na mawakili kupata nafasi ya kujitetea mawakili hao walimwomba hakimu kuwapunguzia hukumu washitakiwa kwani hawakutenda kosa kwa kukusudia na ni mara yao ya kwanza kutenda kosa hilo.

Hata hivyo upande wa waendesha mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) walimuomba hakimu kutoa adhabu kali kwa kuwa vitendo vya ubadhilifu katika halmashauri zimekithili kwa kiasi kikubwa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *