Aliyemuua mwanariadha afariki dunia
KENYA : ALIYEKUWA mpenzi wa mwanariadha Rebecca Cheptegei Dickson Ndiema ameaga dunia katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret.
Hospitali hiyo ilithibitisha kuwa Ndiema alifariki jumatatu ya wiki hii katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) alikokuwa amelazwa.
Ndiema alifariki siku chache baaada ya Cheptegei kufariki katika hospitali hiyo ikidaiwa kuwa alimmwagia mafuta ya petroli kisha kumchoma moto, mbele ya watoto wake wawili.
Polisi walithibitisha kuwa wawili hao wamekuwa na mzozo wa muda mrefu sana kuhusu umiliki wa kipande cha ardhi ambacho Rebecca alikuwa akiishi.
SOMA : Cheptegei atazikwa Jumamosi wiki hii nchini Uganda.