Mwanariadha Cheptegei afariki dunia
MWANARIADHA wa Olimpiki, Rebecca Cheptegei amefariki dunia ikiwa ni siku chache baada ya kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na aliyekuwa mpenzi wake.
Mwanariadha huyo wa Uganda wa mbio za marathon mwenye umri wa miaka 33, ambaye alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya hivi karibuni nchini Ufaransa alipata majeraha makubwa baada ya shambulio hilo.
Mamlaka Kaskazini-Magharibi mwa Kenya, ambako Cheptegei aliishi na kupata mafunzo, zilisema alilengwa baada ya kurejea nyumbani kutoka kanisani na binti zake wawili.
SOMA: Robo fainali EURO 2024 kukamilika leo
Ripoti iliyowasilishwa na msimamizi wa eneo hilo ilidai kuwa mwanariadha huyo na mpenzi wake wa zamani walikuwa wakizozana kuhusu kipande cha ardhi. Polisi wanasema uchunguzi unaendelea.
Kuna wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya ukatili dhidi ya wanariadha wa kike nchini Kenya. Cheptegei ni wa tatu kuuawa tangu Oktoba 2021.