Aljazeeera yafungiwa Congo

CONGO : SERIKALI  ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekifungia kituo cha televisheni cha Al Jazeera kutokana na kurusha mahojiano na kiongozi wa kundi la waasi wa M23 Bertrand Bisimwa.

Msemaji wa serikali ya Congo, Patrick Muyaya amesema mamlaka zimebatilisha kibali cha kurusha matangazo cha televisheni hiyo ya Qatar nchini Congo, baada ya kurusha mahojiano na mkuu wa kundi la M23, Bertrand Bisimwa. SOMA: KAGAME: Rwanda haihusiki kuifadhili M23

Siku ya Jumatano, Al Jazeera ilirusha mahojiano ya Bisimwa, ambapo aliishutumu serikali ya Congo kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwezi Agosti.

Aidha, Waziri wa Sheria wa Congo, Constant Mutamba amesema waandishi wa habari au mtu yeyote atakayeripoti kuhusu shughuli za jeshi la Rwanda na waasi wa M23, atashtakiwa na kuhukumiwa adhabu ya kifo.

Habari Zifananazo

Back to top button