Amani kipaumbele kwa wafanyabiashara ndogo

DAR ES SALAAM: Amani na mshikamano wa kitaifa ni kipaumbele kikubwa kwa vijana wajasiriamali na wafanyabiashara ndogo, huku wakionya kwamba mgawanyiko wa kisiasa na vurugu unaathiri moja kwa moja maisha yao na biashara.

Adam Ally, kijana mwenye biashara ya nguo Sinza, anasema utulivu wa kisiasa unakuza wateja, biashara inakua na inawawezesha kupanga maisha yao. Mgawanyiko au vurugu, anaongeza, hupunguza mauzo na usalama wa wafanyabiashara ndogo.

Christina Joseph, mama lishe wa eneo hilo, anabainisha kuwa hali ya amani inaathiri moja kwa moja mapato yake ya kila siku. Wakati watu wanatembea kwa uhuru, biashara inaendelea, lakini hofu na mvutano hupelekea wateja kupotea na mapato kupungua mara moja. “Kwa sisi wafanyabiashara wadogo, amani si kauli ya kisiasa tu, bali ni kipaumbele cha kuishi,” amesema.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, mchambuzi wa kisiasa na muelezi wa vijana, Masoud Mambo, aliwataka wananchi kujenga demokrasia ya kweli inayojengwa kwa hoja, sera madhubuti na mazungumzo yenye kujenga badala ya vitisho au msukumo wa kisiasa.

“Tanzania inaendeshwa kwa sheria, na vyama vyote vya kisiasa vilivyojisajili kisheria vina haki sawa bila ubaguzi. Kujaribu kuzuia, kutishia au kudhalilisha wanasiasa kupitia taarifa zisizo sahihi au chuki ni kinyume na misingi ya demokrasia, haki na usawa,” Mambo ameongeza.

Mambo pia aliwaonya wananchi juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, akisema kuwa kueneza taarifa zisizo sahihi au propaganda za kisiasa kunadhuru mshikamano wa kitaifa na kuathiri uchumi na diplomasia ya nchi. Aliwataka wananchi, ikiwemo walioko nje ya nchi, kuchangia mshikamano wa kitaifa kwa kutumia mitandao kwa uwajibikaji.

“Tanzania ni yetu sote. Bila amani, haki hazitadumu, bila utulivu, maendeleo hayatafanikiwa, na bila mshikamano wa kitaifa, taifa haliwezi kuwa na nguvu”.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. ᴄᴀꜱʜ ᴇᴀʀɴɪɴɢ ᴊᴏʙ ᴛᴏ ᴇᴀʀɴꜱ ᴍᴏʀᴇ ᴛʜᴀɴ $700 ᴘᴇʀ ᴅᴀʏ. ɢᴇᴛᴛɪɴɢ ᴘᴀɪᴅ ᴡᴇᴇᴋʟʏ ᴍᴏʀᴇ ᴛʜᴀɴ $3500 ᴏʀ ᴍᴏʀᴇ ꜱɪᴍᴘʟʏ ᴅᴏɪɴɢ ᴇᴀꜱʏ ᴡᴏʀᴋ ᴏɴʟɪɴᴇ. ɴᴏ ꜱᴘᴇᴄɪᴀʟ ꜱᴋɪʟʟꜱ ʀᴇQᴜɪʀᴇᴅ ꜰᴏʀ ᴛʜɪꜱ ᴊᴏʙ ᴀɴᴅ ʀᴇɢᴜʟᴀʀ ᴇᴀʀɴɪɴɢ ꜰʀᴏᴍ ᴛʜɪꜱ ᴀʀᴇ ᴊᴜꜱᴛ ᴀᴡᴇꜱᴏᴍᴇ. ᴀʟʟ ʏᴏᴜ ɴᴇᴇᴅ ɪꜱ 2 ʜʀꜱ ᴀ ᴅᴀʏ ꜰᴏʀ ᴛʜɪꜱ ᴊᴏʙ ᴀɴᴅ ᴇᴀʀɴɪɴɢ ᴀʀᴇ ᴀᴡᴇꜱᴏᴍᴇ. ᴇᴠᴇʀʏ ᴘᴇʀꜱᴏɴ ᴄᴀɴ ɢᴇᴛ ᴛʜɪꜱ ʙʏ ꜰᴏʟʟᴏᴡ ᴅᴇᴛᴀɪʟꜱ ʜᴇʀᴇ…

    .

    ᴍᴏʀᴇ ᴅᴇᴛᴀɪʟꜱ ꜰᴏʀ ᴜꜱ ————————➤ join.work43.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button