Amnesty yaitaka Mali kuchunguza mauaji ya raia

MALI : SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limeutaka utawala wa kijeshi nchini Mali kuchunguza mauaji ya raia wanane kufuatia mashambulizi ya droni kaskazini mwa nchi hiyo.

Katika taarifa, Amnesty imesema mashahidi wameripoti kuwa takriban raia wanane, wakiwemo watoto sita, waliuawa katika mashambulizi ya anga kwenye soko lenye shughuli nyingi katika kijiji cha Inadiatafane, katika eneo la Timbuktu Oktoba 21.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu wengine 15 walijeruhiwa huku wengine wakiwa katika hali mbaya.

AMNESTY imesema kuwa shambulizi hilo linapaswa kuchunguzwa kama uhalifu wa kivita kwasababu lilisababisha vifo miongoni mwa raia.

Serikali ya Mali imekuwa ikiendelea kujitetea dhidi ya shutuma  hizo dhidi ya makosa yanayodhuru maisha ya raia.

SOMA: Jeshi la Mali laua magaidi 40

 

Habari Zifananazo

Back to top button