MALI : JESHI la Mali limesema limewauwa magaidi 40 na kuharibu ngome zao katika operesheni mbili zilizofanyika nchini humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Mali nchini humo imesema katika operesheni iliyofanyika Alhamisi na Ijumaa wiki iliyopita katika mji wa Ounguel iliweza kuharibu ngome moja magaidi na kuwaua magaidi 30 huku risasi, silaha na pikipiki 24 zikikamatwa.
Siku ya Ijumaa wiki iliyopita walifanikiwa kuwaua wanamgambo 10 pamoja na kukamata bidhaa ikiwemo magari na pikipiki.
Mali bado inaendelea kukabiliana na migogoro ya kisiasa, usalama na uchumi na imekuwa ikiandamwa na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na lile linalojiita dola la kiislamu tangu mwaka 2012.