Amorim: Najihisi “aibu”

Kocha Mkuu wa Manchester United, Ruben Amorim, amekiri kuwa anajisihisi “aibu” kuongoza timu hiyo katika hali yake ya sasa, akisema Mashetani hao Wekundu wamejikuta wakipambana kujinusuru kushuka daraja.

Kipigo cha mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Newcastle United Desemba 30 kimekiacha kikosi cha Amorim kikiwa katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kikiwa na ponti 22 tu baada ya mechi 19 na kikiwa pointi saba tu juu ya mstari wa kushuka daraja.

SOMA: Man United mtegoni

“Ni aibu kidogo kuwa kocha wa Manchester United na kupoteza mechi nyingi. Hilo liko wazi kabisa, kwa hivyo tunapaswa kupambana. Huu ni wakati mgumu sana, moja ya nyakati ngumu zaidi katika historia ya Manchester United, na tunapaswa kukabiliana nayo kwa uaminifu,” amesema Amorim.

Mchezo unaofuata wa Manchested United EPL utafanyika ugenini Januari 5 dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Liverpool.

Habari Zifananazo

Back to top button