Anastazia atangaza nia Viti Maalum Udiwani Mbweni

DAR ES SALAAM: Anastazia Dinho, mkazi wa Malindi Estate, kata ya Mbweni, ametangaza nia ya kugombea udiwani wa viti maalum kwa lengo la kusaidia wananchi, hasa wanawake na vijana wa mitaani.

“Nimeamua kugombea viti maalum udiwani. Nia na madhumuni ni kwa ajili ya kusaidia wananchi na hasa sisi wanawake. Tunapenda kujitetea katika ngazi mbalimbali na kusaidia vijana wetu wa mitaani,” alisema Anastazia.

Ameeleza kuwa endapo Mungu atamjalia na kufanikiwa kupata nafasi hiyo, atajitahidi kuwasaidia watoto wa mitaani, wanawake na vikundi mbalimbali vya kijamii.

“Inategemea kama Mungu atanijalia nikapata. Ikitokea fadhila hiyo, nitasaidia watoto wa mitaani, hasa wamama na vikundi mbalimbali, hususan wananchi kwa ujumla. Kwa sababu wamama ndio msingi wa familia, wamama ndio chanzo cha familia,” aliongeza.

Anastazia amesema hii ni mara yake ya kwanza kugombea, na anaamini kuwa kama mama ataweza kuwa imara na kutetea wanawake kwa juhudi na nguvu zake zote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button