APR yatangulia fainali Kombe la Dar Port Kagame

KLABU ya APR ya Rwanda imetinga fainali ya michuano ya Kombe la Dar Port Kagame baada ya kuitoa Al Hilal ya Sudan kwa penalti 5-4 kufuatia matokeo ya suluhu ya 0-0 hadi muda wa nyongeza katika nusu fainali ya kwanza kwenye uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. APR sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Al Wadi na Red Arrows itakayopigwa baadaye leo uwanja wa Azam Complex.