WAAMUZI wa Tanzania, Ahmed Arajiga na Frank Komba ni miongoni mwa waamuzi 63 walioteuliwa kuchezesha fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza michuano ya Mataifa ya Afrika ya Ligi za Ndani (CHAN) 2024 itakayofanyika Februari Mosi hadi Februari 28, mwaka huu.
Aragija na Komba wapo katika orodha ya awali ya waamuzi watakaofanyiwa mchujo wa fainali hizo zitakazofanyika Tanzania, Kenya na Uganda.
Katika orodha hiyo waamuzi wa kati ni 25, wasaidizi 22 na 16 ni waamuzi wa teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa (VAR).
Waamuzi wengine wa kati ni Messie Nvoulou, Bito Frank, Malala Yannick, Ouattara Jean, Kpan Franklin, Abdulsalam Abiola, Adissa Ligali, Aklesso Linama, Melki Mehrez, Loutfi Bekouassa, Ahmed Mahmoud, Ahmed Abdulrazg, Kech Mustapha, Rakotojaona Andofetra, Milazare Patrice, Celso Alvacao, Jelly Chavani, Mohamed Athoumani, Nyagrowa Mimisa, Lucky Kasalirwe, Mogos Tsegay, Jammeh Lamin, Diouf Adalbert na Ousmane Diakhate.
Waamuzi wasaidizi wengine ni Ngila Bongele, Rodrigue Mpele, Malondi Yanes, Addy Dodoo, Oumar Sanou, Samuel Pwadutakam, Yacouba Aziz, Nassiri Hamza, Adel Abane, Wael Hanachi, Amaldine Soulaimane, Lucky Kegalogetswe, Mutuyimana Dieudonne, Fasika Yehualashet, Omer Ahmed, Emery Niyongabo, Mwangi Kuria, Ronald Katenya, Joel Doe, Diba Hamedine na Jawo AbduAziz.
Kwenye VAR ni Kabore Vincent, Abou Coulibaly, Brahamou Sadou, Boukhalfa Nabil, Hamza El Fariq, Haggag Ibrahim, Badi Luxolo, Ngakosso Chancelle, Nguiene Pierre, Brighton Chimene, Abdalaziz Ahmed, Dintwa Keabetswe, Twagimurukiza Abdoul, Sarr Ababacar na Diou Moussa.
Arajiga ni mwamuzi bora wa Ligi Kuu msimu uliokwisha na Komba ni mwamuzi bora msaidizi kwa misimu minne mfufulizo.