TETESI za usajili zinaonesha Arsenal ina shauku kumsajili winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams, 22, na kiungo wa Real Sociedad, Mikel Merino, 28, lakini inakabiliwa na ushindani toka Barcelona kwa ajili ya wachezaji hao wa kimataifa wa Hispania.
Williams amekuwa mojawapo ya majina yanayozungumziwa mno katika soko la uhamisho.
Akitambulika kwa kasi yake ya ufundi, na uwezo wa kuwashinda mabeki, Williams amevutia macho ya miamba kadhaa ya soka Ulaya.
Umahiri wa uchezaji wake Ligi Kuu Hispania-La Liga na timu ya taifa ya Hispania umeonyesha uwezo wake wa kuwa mmoja wa mawinga bora barani Ulaya.
SOMA: Erling Haaland, Nico Williams kutua Barcelona
Kiwango chake kimesababisha uvumi kuhusu mustakabali wake, huku timu kama Liverpool, Manchester City, na Bayern Munich zikiripotiwa kuwa na nia kubwa ya kumsajili. Sakata la uhamisho linalomzunguka Williams limechochewa na umri wake mdogo na uwezo wa kukua zaidi.
Akiwa na umri wa miaka 22 pekee, Williams tayari ameonesha ukomavu uwanjani zaidi ya umri wake, jambo linalomfanya kuwa rasilimali ya thamani kwa timu yoyote inayotaka kuwekeza kwa mchezaji mwenye kiwango cha juu cha ukuaji.
Mkataba wake wa sasa na Athletic Bilbao unajumuisha kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 48.7 ambacho kimeongeza ugumu katika mazungumzo.
Vilabu vinavyomwinda Williams vitahitaji kufikia kiwango hicho cha kuachiliwa au kujadiliana kwa faida na Bilbao, ambao wanataka kumbakiza nyota wao lakini pia wanatambua athari za kifedha za uhamisho wa kiwango cha juu.

Borussia Dortmund, Juventus na Paris Saint-Germain zina nia kumsajili fowadi wa Manchester United Jadon Sancho, 24, lakini haziwezi kutimiza thamani ya mchezaji huyo iliyowekwa na klabu hiyo ya Old Trafford. (Sky Sports)
United inataka ada ya pauni milioni 40 kwa ajili ya Sancho. (Mirror)

Manchester City ipo katika mazumgumzo kumuuza beki wa kulia wa Brazil, Yan Couto, 22, ambaye bado hajacheza klabu hiyo kwenda Borussia Dortmund na inatarajia klabu hiyo ya Ujerumani kutoa ofa ya karibu pauni milioni 25.(Mail)
Beki wa kati wa Newcastle United Kieran Trippier, 33, anawaniwa na klabu mbili za Saudi Arabia na huku mwaka mmoja umebaki katika mkataba wake, anatarajiwa kuondoka klabu hiyo ya Tyneside. (Northern Echo)