Arsenal yapeleka £23m kwa Raya
ARSENAL sasa imewasilisha ofa rasmi ya pauni 20 na nyongeza ya pauni 3 kwa ajili ya kuinasa saini ya kipa David Raya kutoka Brentford.
Licha ya dau hilo ambalo Brentford hawajalikubali bado, taarifa ya Fabrizio Romano aliyotoa siku mbili zilizopita ilieleza thamani ya Raya ni £40m.
Makubaliano binafsi kati ya mchezaji huyo na Arsenal yameafikiwa tayari, hivyo klabu hiyo inasubiri majibu ya dau hilo kuona kama watamnasa.
Aaron Ramsdale na Matt Tuner ndio makipa wa Arsenal kwa sasa, ujio wa Raya unakuja kutoa changamoto kwa wawili hao.