Arteta, Saka watwaa tuzo Machi

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amechaguliwa na Shirikisho la soka England ‘FA’ kuwa kocha bora wa mwezi Machi kwa mara ya nne msimu huu.

Mshambuliaji wa timu hiyo, Bukayo Saka pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora kwa mara ya kwanza.

Arteta alitwaa tuzo hiyo mwezi August, November/ Disemba, Januari na Machi.

Saka ameshinda tuzo hiyo baada ya kufunga mabao matatu na kutoa pasi za mabao mawili katika michezo minne ambayo yote Arsenal ilishinda.

Habari Zifananazo

Back to top button