Arusha, Manyara ukeketaji asilimia 43

DODOMA; Mikoa ya Arusha na Manyara bado ina kiwango kikubwa cha ukeketaji ukilinganisha na mikoa mingine nchini.

WAZIRI wa Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima, amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2024/2025.

Ametaja mikoa na asilimia yake ya ukeketaji katika mabano ni Arusha (43%), Manyara (43%), Mara (28%), Singida (20%), Tanga (19%), Dodoma (18%), Iringa (12%), Morogoro (10%), Kilimanjaro (9%), Njombe (7%), Pwani (5%) na Mbeya (3%). Mikoa mingine, ukeketaji upo chini ya asilimia 1.

Amesema takwimu za hali ya afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria Tanzania za mwaka 2022/2023 zinaonesha kupungua kwa vitendo vya ukeketaji nchini kutoka asilimia 10 kwa mwaka 2015/2016 hadi asilimia 8 kwa mwaka 2022/2023.

Amesema wizara inaendelea na utekelezaji wa mkakati huo, ili kufikia lengo la kupunguza vitendo vya ukeketaji hadi asilimia 5 ifikapo mwaka 2025.

Habari Zifananazo

Back to top button