Arusha sensa wafikia asilimia 99

Arusha

MKOA wa Arusha umefikia asilimia 99.5 ya kaya zilizotakiwa kuhesabiwa katika zoezi la sensa ya watu linalotarajiwa kumalizika leo usiku

Mkoa wa Arusha umefanikiwa kuhesabu kaya zaidi ya 562,300 kati ya kaya 565,800,  ambapo ni sawa na asilimia 99.5

Akizungumza leo jijini Arusha, Msimamizi wa Sensa Mkoa wa Arusha, Mloka Omari alisisitiza zoezi hilo kwa mkoa wa Arusha linakwenda vizuri  hadi leo jioni.

Advertisement

Amesema hadi juzi jioni kaya 562,300 ndio zimefikiwa na wanatarajia ongezeko la kaya hizo litakuwepo, sababu wameongeza nguvu kuhakikisha wananchi wanahesabiwa