Arusha Warriors yaahidi makubwa soka walemavu

TIMU ya Arusha Warriors imekusudia kufanya vizuri katika mashindano ya soka kwa walemavu yatakaoanza Julai 17 hadi 19 katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.

Arusha Warriors inashiriki mashindano hayo kwa mara ya pili ambapo mwaka 2023 ilifanikiwa kuwa mshindi wa pili

Michuano ya soka kwa walemavu inayojulikana Azam Amputee Football Tournament 2025 imeandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF)”

Timu hiyo inaondoka leo kuelekea jijini Dara es Salaam ambapo kampuni ya Bonite Botllers limited imetoa msaada wa maji kwa ajili ya timu hiyo ambayo itawakiliwa na msafara wa watu 15 ,wachezaji 12 na viongozi 3.

Akizungumza wakati wa kukabidhi katoni za maji kwa timu hiyo Msimamizi kutoka kampuni ya Bonite bottlers, Hamza Ally amesema siku zote bonite imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia michezo pia kurudisha kwa jamii na msaada kama huo ni mdogo lakini wanaimani utasaidia timu hiyo katika mashindano na kuwatakia wachezaji safari njema huko waendako waende wakapambane na tunatarajia watarudi na ushindi.

Naye Elias Saimon kocha wa timu hiyo alimshukuru Ofisa michezo wa jiji kwa kuonyesha moyo mkubwa na kusaidia kwa namna moja katika kuona timu yao inaenda kushiriki mashindano hayo.

“Vijana wangu walikufa moyo lakini sasa wanajitoa na nimewaambia kwamba wasikate tamaa na jamii itambue ukiwa mlemavu sio kwamba huwezi kufanya kitu hivyo tunaenda kwenye michezo kwa ari kubwa ya kufanya vizuri,”amesema Saimoni.

Kwa upande wake, mwenyekiti msaidizi wa timu hiyo Alloyce Sabuni ameeleza kuwa wamejipanga kikamilifu na timu ina malengo makubwa ya kwenda kufanya vizuri na amewaomba wadau kuendelea kuwaunga mkono kwani bado changamoto za ukosefu wa vifaa vinawakabili.

Ofisa Michezo wa jiji la Arusha, Benson Maneno amesema wanatambua umuhimu wa mashindano haya kwa jamii yetu na michezo ya watu wenye ulemavu hivyo Serikali ya jiji la Arusha itaendelea kutoa sapoti kupitia vifaa vya michezo na rasilimali nyingine muhimu na ameishukuru Bonite Botllers kwa mchango wao.

Mashindano hayo yanajulikana kama Azam Amputee Football Tournament 2025 yameandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF),yakihusisha vilabu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na timu mwalikwa kutoka nje ya nchi lengo likiwa ni kukuza na kuendeleza mchezo wa soka kwa watu wenye ulemavu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button