Asilimia 70 watu wamekufa Gaza

PALESTINA : OFISI ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema asilimia 70 ya watu waliouawa vitani katika ukanda wa Gaza ni wanawake na watoto.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja huo wa Mataifa Volker Türk, amesema takwimu zinaonyesha kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Turk amelaani vikali kuhusu matatizo yanayoendelea  katika ukanda wa Gaza na kudai kuwa kunahaja ya kuhifadhi taarifa hizi ili zije zitumike kama ushahidi katika vyombo vya sheria.

Advertisement

Kwa mujibu wa Shirika la utangazaji  Reuters mpaka sasa  ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hawajaweza kutoa taarifa kuhusu taarifa za takwimu hizi.

SOMA: Raia Gaza waingia hofu kusitishwa UNRWA