Askofu Mdoe atoa wito kumfuata Mungu

MTWARA: Mhashamu Titusi Mdoe Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara, amewataka waumini kuendelea kufuata njia za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.

Akizungumza wakati wa hitimisho la maadhimisho ya Jubilei ya miaka 50 ya Parokia ya Mtakatifu Paul Majengo Jimbo Katoliki Mtwara tangu kuanzishwa kwake, Askofu Mdoe amesema watu waendelee kumtukuza Mungu kwa imani na matendo yao.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Parokia ya Mtakatifu Paul Majengo, Jimbo Katoliki Mtwara ambapo Jubilei hiyo ilizinduliwa Aprili 14,2024.

‘’Niendelee kumwomba na kumshukuru Mwenyezi Mungu, aendelee kuwatia nguvu waumini wa parokia hii, jubilei pamoja na kanisa letu la Tanzania kwa ujumla na dunia mzima ili watu waendelee kumtukuza Mungu kwa imani yao na matendo yao’’amesema Askofu Mdoe.

Amesema katika kusherehekea huko wanapata fursa kama wanakanisa na kama sehemu ya taifa kwa kuendelea kusali na kumwomba Mungu ili awaweke salama, kuwaleta karibu watanzania, awaondolee matatizo yasiyokuwa ya lazima katika nchi yao.

Kwa upande wao baadhi ya waumini wa Kanisa hilo akiwemo Grace Tandesi amesema amefurahishwa na uwepo wa siku hiyo kwasababu anashuhudia matendo makuu ya Mungu huku akiwaomba waumini na wakristu wengine duniani kuwa, wasiache imani yao na wasiyumbishe na imani zingine zisizotakiwa katika uumini wao.

Mwenyekiti wa Kigango cha Roho Mtakatifu Mangamba CPA Norbert Shee amesema katika mambo wanayopaswa kujifunza ikiwemo waumini kuanza kuelewa kwamba kujenga Kanisa ni jukumu lao na siyo kutegemea misaada kutoka kwa wengine huku akiwaomba kuendelea kueneza injili kwa imani na matendo yaliyokuwa mema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button