GEITA; ASKOFU wa Jimbo Katoliki, Dayosisi ya Rulenge Ngara, Askofu Severine Niwemugizi ameongoza ibada ya Misa Takatifu ya kumkumbuka na kumuombea Rais wa Awamu ya Tano, hayati Dk John Pombe Magufuli.
Ibada ya Misa hiyo imefanyika leo Machi 17, 2025 katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria Mzeyi, Mlimani wilayani Chato mkoani Geita kuadhimisha miaka minne ya kifo cha hayati Dk Magufuli.
Ibada imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, chama na serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, William Lukuvi pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa.
Aidha wanafamilia wameongozwa na mjane wa Dk Magufuli, Mama Janeth Magufuli. Pia wananchi mbalimbali wamehudhuria.