Ataka bodaboda, bajaji wabanwe kuzuia ajali

KITUO cha umahiri wa usalama barabarani kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini kimetaka sheria za usalama barabarani zisimamiwe madhubuti ili kuhakikisha waendesha pikipi za abiria maarufu bodaboda na bajaji wanapata elimu ya usalama barabarani na kuwa na leseni kabla kukabidhiwa vyombo vya moto ili kusaidia kudhibiti ajali za barabarani.

Mkuu wa kituo cha umahiri wa usalama barabarani Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, Godlisten Msumanje alisema hayo mjini Kasulu katika mfululizo wa elimu kwa waendesha vyombo vya moto barabarani  ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabarani ya lami kutoka Manyovu Wilaya ya Buhigwe hadi Kabingo wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

Advertisement

Amesema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazojitokeza barabarani ni kutofuatwa kwa  matumizi sahihi ya sheria za barabara na alama za usalama barabarani hivyo madereva wa vyombo vya moto ambao hawajapitia kwenye vyuo vinavyotoa elimu hiyo wamekuwa changamoto kubwa hivyo wamiliki wa vyombo wanapaswa kuhakikisha kuwa wanaoendesha vyombo hivyo wana sifa zinazotakiwa na serikali.

Msumanje amesema kuwa serikali inatumia gharama kubwa katika kuimarisha miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji lakini mwendo kasi na uzembe barabarani vimekuwa changamoto kubwa katika kufanya ajali za barabarani ziendelee lakini madereva ambao hawakupata elimu ya usalama barabarani wamekuwa wakiongeza tatizo kwenye jambo hilo.

Akizungumza katika elimu hiyo kwa madereva askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Emanuel Fusi amesema kuwa bado ipo idadi ya kutosha ya madereva wa bodaboda na bajaji ambao wanaingia barabarani kuendesha vyombo vya moto bila kupitia mafunzo ya usalama barabarani na ndiyo wanachangia ongezeko la ajali hasa kwa wanafunzi na watoto.

Baadhi ya waendesha bodaboda na bajaji waliohudhuria mkutano huo wa kutoa elimu ya usalama barabarani wilayani Kasulu akiwemo, Emanuel Paul alisema kuwa inaweza kuwa jambo jema kama waendesha vyombo vya moto watabanwa kuhakikisha wanapitia kwenye vyuo  ili kujua vizuri sheria na alama za barabarani ili kuzuia ajali ambapo amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya bodaboda ambao wanafanya kazi hiyo wakiwa hawana leseni.

1 comments
  1. Womderful article! Thiss iis thhe kind of info that are supposed to bee shared across the internet.
    Shame on thhe seasrch enginees for nott positiuoning ths
    post higher! Coome on ovver aand alk oer
    with myy web sote . Thank you =)

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *