Ataka ufafiti maeneo mengine ya madini

NAIBU Katibu  Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo  ametoa wito kwa  Kampuni ya Stamigold kupitia Mgodi wa Biharamulo Mine,  kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), kufanya tafiti zaidi, ili kubaini maeneo mengine yenye mashapo kwa lengo la kuongeza maisha ya mgodi huo.

Naibu huyo alitoa wito huo wakati wa ziara yake katika mgodi wa kuchimba dhahabu  Biharamulo Mine, iliyolenga kukagua uzalishaji, kufanya kikao na watumishi, kuangalia afya za wafanyakazi na usalama mahali pa kazi.

Baada ya kupokea taarifa katika uongozi wa mgodi huo, alisisitiza mgodi huo  kuendelea kufanya utafiti zaidi kwa maeneo ambayo hayajachimbwa dhahabu kuona kama uhai wa mgodi unaweza kuongezeka.

Alisema kuwa mgodi wa Biharamulo Mine unamilikiwa kwa asilimia 100 Stamigold ambayo ni Kampuni tanzu ya Shirika ya Madini la Taifa (STAMICO), inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera na kupitia ziara hiyo amefurahishwa na Watanzania kufanya kazi kwa weledi kuanzia ngazi ya utafiti hadi kuongeza thamani ya madini mpaka kupelekwa sokoni.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Stamigold, Ally Ally alisema kuwa mpaka sasa utafiti uliofanyika mwaka wa Fedha 2022/2023 kuhusu uhai wa mgodi huo ni kuwa eneo lililofanyiwa utafiti  inaonesha Kampuni hiyo itaendelea kuchimba madini hadi miaka 5 ijayo, huku akisema kuwa nguvu kubwa itatumika kufanya utafiti  wa sehemu ambayo haijachimbwa madini kujua aina za madini zilizopo.

Alisema kuwa uzalishaji wa dhahabu katika mgodi wa Biharamulo Mine unazidi kuimarika mwaka hadi mwaka, ambapo kwa sasa zaidi ya kilo 50 mpaka 60 zinazalishwa kwa mwezi, ukilinganisha na kilo 35 mpaka 40 miaka iliyopita, huku maeneo yalizunguka mgodo huo yakinufaika na huduma za jamii kama afya, elimu, ujasiriamali na ajira za muda mfupi.

Alisema  mgodi huo unachimbwa na Watanzania kwa asilimia 100, ambapo imeajiri watumishi 566, ikiwa 232 wameajiriwa na Stamigold, 238 ni wanafunzi kutoka vyuo vikuu na taasisi nyingine na 80 ni kutoka kwenye jamii ya wakazi waliozunguka mgodi  huo .

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button