ATCL yarejesha safari za ndege Dar- Guangzhou

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), limerejesha safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou China kuanzia Mei 11, 2023.

Kupitia ukarasa wao wa twitter @AirTanzania safari zitafanyika  mara tatu kwa wiki kwa siku za Jumanne, Alhamis na Jumamosi kutokea Dar es Salaam (Tanzania) na Jumatano, Ijumaa  na Jumapili kwa kutokea Guangzhou (China).

Kupitia ukurasa wa twitter wa ubalozi wa Tanzania nchini China  @TZEmbassyCN Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amewataka abiria kutumia usafiri wa shirika hilo kwani ni rahisi na unatumia takribani ya masaa kumi.

“Nitoe rai kwa abiria wanaopenda kusafiri kuja China kwa ajili ya shughuli za biashara, mafunzo au kikazi basi watumie Shirika la Ndege la Tanzania,” ulisomeka ujumbe huo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian  kupitia ukurasa wake wa twitter @ChenMingjian_CN, amesema amefurahishwa na kurejea kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania za kwenda na kurudi kati ya Dar es Salaam na Guangzhou, kwani litakuza biashara na utalii kupitia mabadilishano ya watu kati ya China na Tanzania.

“Nimefurahi kuona  kuwa @AirTanzania  itaanza tena safari zake za za kwenda na kurudi kati ya Dar es Salaam na Guangzhou na kurejea Dar es Salaam kupitia Zanzibar kuanzia Mei 11 2023…

“Tunatumaini shirika hili la ndege linaweza kukuza biashara na utalii kupitia mabadilishano ya watu kati ya China na Tanzania,” unasomeka ujumbe huo.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button