Ateba: Nitafunga sana tu!

DAR ES SALAAM – MSHAMBULIAJI wa Simba, Leonel Ateba amesema kazi iliyomleta Tanzania ni kufunga kila anapopata nafasi ya kucheza ili kuisaidia timu yake kufikia malengo yanayotarajiwa.

Amesema kabla ya kusajiliwa na Simba kuna ofa nyingi zilizofika mezani kwake lakini aliamua kuachana nazo na kujiunga na Simba kwasababu anaamini soka la Tanzania lina ushindani mkubwa.

Ateba alisajiliwa na Simba dirisha kubwa la usajili lililopita akitokea klabu ya USM Alger ya Algeria kwa mkataba wa miaka miwili.

Ateba amesema kazi kubwa iliyopo mbele yake ni kufunga bao katika kila mchezo anapopata nafasi ili kuendelea kuwapa furaha mashabiki wa Simba ambao wanakuwa kila sehemu kuwasapoti. “Nimeona hamasa waliyonayo mashabiki, wanaonesha wana kiu ya mafanikio.

Sisi kama Wachezaji, msimu huu tutapambana sana kwa ajili yao, binafsi nitahakikisha nafanya vizuri katika kila mchezo kwa kufunga mabao,” amesema Ateba.

SOMA: Kiduku apoteza pambano kwa pointi Ulaya

Straika huyo amesema, ana furaha kubwa kuona timu yao imeingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika akiamini kwamba, wanao uwezo mkubwa wa kupambana na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwani wana kikosi kizuri.

Tayari staa huyo ameshaanza kuonesha makali yake akiivusha Simba kwenda hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-1 na Al Ahli Tripoli ya Libya pamoja kufunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC.

Habari Zifananazo

One Comment

Back to top button