MAREKANI : UMOJA wa Afrika umesikitishwa na uamuzi wa Marekani kujiondoa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Hivi karibuni, Rais Donald Trump alisaini amri ya kiutendaji ambayo inatekeleza hatua ya kujiondoa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa. SOMA: Trump kusitisha kazi za watu zaidi ya 1000
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat alisema, “tangazo la serikali ya Marekani la kujiondoa WHO tumesikitishwa sana.”
Washington ni mchangiaji mkuu wa kifedha kwa shirika hilo, na kujiondoa huku kunakuja wakati ambapo Bara la Afrika linakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiafya, ikiwemo milipuko ya hivi karibuni ya virusi vya mpox na Marburg.