Aweso ahimiza uchaguzi serikali za mitaa

MBUNGE wa Jimbo la Pangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jumaa Aweso amesema Tanzania ni nchi ya kidemokrasia hivyo uchaguzi ni namna nzuri ya kupata viongozi huku akiwahimiza wananchi kujiandikikisha kwenye daftari la kupiga kura.

Aweso ambaye ni Waziri wa Maji amesema hayo leo Oktoba 17, 2024  mara baada ya kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura katika kijiji alichozaliwa cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani huku akileza kwamba ni muhimu wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.

Amesema ni muhimu wananchi wakatumia muda uliowekwa kwa ajili ya kujiandikisha na ili kupata viongozi ambao wanawataka lakini wakaowaleta maendeleo.

“Leo nimejiandikisha kwenye kijiji changu ili apate haki ya msingi kupata kiongozi anayemtaka ambaye atashirikiana na wengine kuleta maendeleo nitoe wito wananchi Pangani na watanzania tujitokeza kujiandilisha na kupiga kura ili kupata viongozi ambao wanashirkiana na Rais katika kuleta maendelelo katika vijiji vyetu,” amesema Jumaa Aweso.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Gift Macha amesema mpaka sasa wameweza kufikia asilimia 60 ya uandikishaji wananchi lakini hamasa zinaendelea zaidi katika kuhakikisha wanafikia malengo ya zaidi ya asilimia 100.

Habari Zifananazo

Back to top button