Aweso akabidhi vitendea kazi DAWASA

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amekabidhi vitendea kazi kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Vifaa vilivyokabidhiwa DAWASA ni kwa dhumuni la kuimarisha utendaji kazi wa watumishi.

SOMA: Dawasa wapewa maagizo matano

Waziri Aweso amekabidhi magari mawili aina Toyota Hilux (pick up), magari ya majitaka sita, pikipiki za magurudumu matatu (bajaji) 25, pikipiki za magurudumu mawili 200 pamoja na maguta 10 yatakayotumika kufanikisha ubebaji na kutoa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo ya huduma ya DAWASA.

Waziri Aweso amewataka watumishi wote wa DAWASA kuongeza juhudi na ufanisi pamoja na kuwa waaminifu katika kazi zao kila siku ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button