Aweso aridhishwa na mradi wa maji Buhigwe
Apokelewa kwa kishindo
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amekagua mradi wa Maji Migongo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
Aweso, ameridhishwa na utekelezaji wake na kuwapongeza wahandisi wa maji RUWASA kwa kazi nzuri.
Mradi huo ambao unanufaisha wananchi 14,242, unagharimu kiasi cha sh. Billion 1.1 na sasa umekamilika kwa asilimia 94 na tayari unatoa huduma ya maji kwa wananchi wa Kijiji cha Migongo.