Aweso asisitiza ubora miradi ya maji miji 28

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amekutana na makandarasi wanaotekeleza mradi wa maji kwenye miji 28 na kuwataka wazingatie ubora.

Alikutana na makandarasi hao juzi ofisini kwake mkoani Dodoma kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mradi huo wa Dola za Marekani milioni 500.

Mradi huo ni moja ya mradi mkubwa wa maji wa kimkakati hapa nchini na unafanikishwa na serikali kupitia mkopo nafuu kutoka serikali ya India kupitia Benki ya Exim ya India.

Aweso aliwataka makandarasi hao kuwa makini katika utekelezaji wa kazi hiyo muhimu ya kuwapatia Watanzania huduma ya majisafi.

Aliwataka makandarasi hao kufanyakazi kwa nguvu kubwa kwa sababu mradi huo umesubiriwa kwa muda mrefu.

Aweso aliwaeleza kuhusu matarajio ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alishuhudia utiaji saini wa mradi katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma hivi karibuni.

Utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 ulianza Aprili 12, 2022 baada ya serikali kukamilisha taratibu za masuala ya kodi na kulipa malipo kwa makandarasi ambao sasa hivi wametawanyika katika maeneo yaliyo katika mpango na kazi imeanza.

Habari Zifananazo

Back to top button