WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewasili jijini Arusha kwa ajili ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama ikiwa ni siku moja tu baada ya maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi kutoka kwa Katibu wa NEC Itikati, Uenezi na Mafunzo CCM, Paul Makonda.
Moja ya changamoto aliyokutana nayo kwa wananchi ni kutopokelewa simu wanapowapigia kitengo cha huduma kwa wateja AUWSA, kero hiyo ilimfanya Waziri Aweso kuwapigia simu kitengo hicho na kutokupokelewa
Sambamba na hilo Aweso amehoji idadi ya watu walioomba kuunganishiwa huduma ya maji ambapo ni wateja 428 kiutaratibu mtu anapoomba kuunganishiwa maji ni ndani ya siku saba lakini bado hawajaunganishiwa huduma hiyo
Amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Maji AUWSA Mhandisi Richard Masika kukaa na menejimenti na kuwapa maelekezo juu ya eneo hili la huduma kwa wateja na kulichukulie hatua na eneo la maunganisho
Aweso amewataka AUWSA kuhakikisha wanaboresha huduma na kutatua changamoyo zilizoonekana kwa haraka ikiwa ni maunganisho mapya ya huduma ya maji kwa wateja malalamiko ya muda mrefu, huduma kwa wateja isioridhisha na upotevu wa maji
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Arusha AUWSA Mhandisi Justine Rujomba amekiri baadhi ya vitengo kutokufanya kazi yao ipasavyo akitolea mfano kitengo cha huduma kwa wateja kutokupokea siku hivyo ametoa ahadi kwa Waziri wa Maji na wananchi kufanya mabadiliko ya vitengo mbalimbali na kuondoa watu wazembe ikiwa ni pamoja na kutengeneza mpango kazi mpya.