Azam vs Simba: Ni kisasi ‘dabi’ ya Mzizima
ZANZIBAR: MACHO na masikio ya wapenda soka leo yataelekea visiwani Zanzibar ambako Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kwa mcheo mmoja wa kibabe wa dabi ya Mzizima kati ya Azam na Simba.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja New Amaan, Unguja.
Mbungi hiyo ni ya kisasi kwani katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Mei 24, Azam ilikubali kipigo cha mabao 3-0 mbele ya Simba kwenye uwanja wa Benjamin, Dar es Salaam.
Azam ipo nafasi 3 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 4 wakati Simba inashika nafasi ya 6 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 2.