MIAKA miwili baada ya kuuawa, mwanaharakati wa upinzani nchini Zimbabwe Moreblessing Ali hatimaye amezikwa katika Mji wa Chitungwiza, Harare.
Ali mwanachama wa chama cha upinzani cha Citizens Coalition for Change (CCC) alitekwa nyara mwaka 2022 nje ya baa moja huko Nyatsime, kitongoji cha Chitungwiza.
Mwili wake uliokuwa umekatwa vipande vipande, ulipatikana wiki mbili baadaye ukiwa umefichwa kisimani.
Familia ya Ali ilikataa kuzika mabaki yake hadi Joe Sikhala, ofisa mkuu na wakili wa familia, alipoachiliwa.
Alikamatwa baada ya kusema kuwa aliuawa na wafuasi wa chama tawala cha Zanu-PF na kukaa karibu miaka miwili kizuizini kabla ya kesi kufunguliwa kabla ya kuachiliwa mwezi Januari baada ya hakimu kusitiaha kifungo.