Baba aua watoto wawili akidai amebambikwa

mshumaa

JESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watuhumiwa wanne ambao ni Junge Jilatu na wenzake watatu wakazi wa Kijiji cha Namsinde, Kata ya Mkulwe kwa tuhuma za mauaji ya watoto wawili.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga ime sema tulio hilo limetokea Januari 11, 2025 saa 2:20 usiku nyumbani kwa mtuhumiwa katika Kijiji cha Namsinde.

Senga alisema mtuhumiwa aliwakaba kwa kamba watoto wake wakiwa wamelala na kisha kuwachoma na kitu chenye ncha kali shingoni.

Advertisement

Senga alibainisha chanzo cha mtuhumiwa kufanya mauaji hayo kuwa ni msongo wa mawazo.

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hili ni msongo wa mawazo baada ya baba wa watoto hao kumtuhumu mke wake kuwa amezaa na ndugu wa karibu wa familia yake,” ilisema taarifa hiyo.

Kamanda Senga alitaja majina ya watoto waliouawa ni Lwambo Charles (3) na Kamba Charles (miezi miwili) ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo mtoto mmoja alimtupa kwenye mtaro wa maji kandokando ya barabara inayokwenda Namsinde.