Baba Levo: Nandy, Zuchu hakuna bifu
MSANII wa Bongo Fleva nchini Revocatus Chipando ‘Baba Levo’ amesema kuwa hakuna bifu lolote linaloendelea baina ya Faustina Mfinanga ‘Nandy’ na Zuhura Othuman ‘Zuchu’.
Baba Levo amesema anachojua Nandy na Zuchu ni marafiki na huwa mara nyingi anawaona wakiwa pamoja.
Pia amezungumzia suala la ‘Zuchu’ kushiriki katika Tamasha la Nandy Festival kama wasanii wengine wanavyo tangazwa kuburudisha.
“Kwanza nimekuta kwenye utambulishinwa wasanii na mimi ni miongoni mwa wasanii watakao burudisha nipo hapa boss wangu Diamond Platnumz anajua na ameniruhusu kasema nenda kamsapoti Nandy anapambana.”
“Lakini pia Zuchu atashiriki kuburudisha katika Mkoa wowote atakaoitajika kwenda kuwaburudisha watanzania atawaburudisha kwa gharama yoyote watakayo kubaliana.”amesema Baba levo