Baba mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mwanaye Geita

JESHI la Polisi mkoa wa Geita linamshikilia Msauzi Bakari (34) mkazi wa kijiji cha Uyovu wilayani Bukombe kwa tuhuma za kumuingilia kimwili mwanaye wa kumzaa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Safia Jongo amebainisha hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Kamanda Jongo amesema mtuhumiwa ni mchimbaji mdogo wa madini ambapo anatuhumiwa kwa kosa la kuzini na maharimu(ndugu) na tukio hilo limebainika Juni 14, 2024 usiku.

Ameeleza, mtoto huyo wa kike mwenye umri wa miaka mitano (jina linahifadhiwa) alithibitishwa kufanyiwa ukatili huo na baba yake katika zahanati ya kijiji cha Uyovu.

Kamanda Jongo amesema baba huyo alimfanyia kitendo hicho mwanaye baada ya kumlaghai kwa zawadi ndogo ambapo uchunguzi umekamilika na punde mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Habari Zifananazo

Back to top button