Baba na mama wa kambo wahukumiwa kifungo cha maisha jela

UINGEREZA : MAHAKAMA moja ya Uingereza imewahukumu maisha baba na mama wa kambo kwa mauaji ya mtoto wa miaka 10, Sara Sharif ambaye raia wa Uingereza mwenye asili ya Kipakistani.
Sara alikufa baada ya kuteswa kwa muda mrefu, na mwili wake ulipatikana ukiwa na majeraha makubwa.
Urfan Sharif, mwenye umri wa miaka 43, alihukumiwa kifungo cha miaka 40, huku mkewe Beinash Batool, mwenye umri wa miaka 30, akihukumiwa kifungo cha miaka 33.
Mahakama ilielezwa kuwa mwili wa Sara ulipatikana na majeraha makubwa, ikiwa ni pamoja na mifupa iliyovunjika na majeraha ya kuchomwa na pasi.
Jaji John Cavanagh alisema kuwa Sara alikuwa muathirika wa mateso ya kupitiliza na kwamba Sharif na Batool hawakuonyesha dalili za kujutia matendo yao.
Alikutwa akiwa amekufa kitandani mwake mwezi Agosti 2023 akiwa peke yake nyumbani. SOMA:Ubize wa wazazi, mmomonyoko wa maadili unavyowaweka watoto hatarini
Uchunguzi wa maiti ulionyesha kuwa Sara alikuwa na majeraha 71 na mifupa 25 iliyovunjika.
Mjomba wake, Faisal Malik, mwenye umri wa miaka 29, alikutwa na hatia ya kusaidia au kuruhusu mauaji hayo kutokea na amehukumiwa kifungo cha miaka 16.



