Bajeti Wizara ya Nishati yapita kwa kishindo

DODOMA: Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha shilingi trilioni 2.53 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati 2026/2027.
 
Kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 2.46 sawa na asilimia 97.5 ya bajeti yote imeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na asilimia 2.5 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
 
Akihitimisha hoja kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2026/2027 Waziri wa Nishati,Deogratius Ndejembi alilieleza Bunge kuwa Wizara ya Nishati itaendelea kuhakikisha kwamba maono ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi na mwelekeo uliowekwa kwenye Dira 2050 yanatekelezwa kwa vitendo na kwa haraka.
 
Kutokana na hilo alieleza kuwa lengo lililowekwa kwa wizara la kuzalisha umeme wa megawati 8000 ifikapo 2030 litatekelezwa kwani Wizara ya Nishati imeshajipanga kuzalisha kiasi hicho cha umeme huku ikidhamiria kuzalisha megawati 70,000 ifikapo 2050.
 
“Ili kutekeleza lengo hili tutatumia vyanzo vyote vinavyopatikana kwenye Taifa letu ikiwemo vyanzo vya maji kama vile Malagarasi (49.5MW), Kakono (87MW), Ruhudji (358), Rumakali (222MW), Jeothemo na makaa ya mawe..” Alisema Ndejembi
 
Akifafanua kuhusu mradi wa uzalishaji wa umeme wa makaa ya mawe, Ndejembi alisema Tanzania ina hifadhi kubwa ya makaa hayo na sasa Serikali inashirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa inaanza uzalishaji wa megawati zaidi ya 2000 kwa kutumia nishati hiyo.
 
Aliongeza kuwa miradi mingine itakayowezesha kufikia lengo la uzalishaji wa megawati 8000 ifikapo 2030 ni pamoja na miradi ya umeme Jua ikiwemo ya Kishapu, Manyoni, Zuzu, miradi ya upepo ya Same, Makambako pamoja na kuzalisha umeme kwa kutumia urani.

Aidha, Ndejembi aligusia suala la kufikisha umeme kwenye maeneo ya wananchi akieleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha umeme unatoka kwenye vyanzo vya uzalishaji na kufikia maeneo ya wananchi na ya uzalishaji kama vile migodi viwanda.

Katika jitihada hizo za kufikisha umeme kwa wananchi alisema mradi wa kufikisha umeme wa gridi mikoa ya Mtwara na Lindi kupitia ujenzi wa njia ya umeme ya kV 220 ya Songea- Tunduru- Masasi-Mahumbika unaendelea huku mkandarasi akiwa ameshalipwa shilingi bilioni 83 kwa ajili ya kuendelea na kazi.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nishati aliiagiza TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) kuwasiliana na Wabunge wote ambao wana maeneo ambayo ni Manispaa/Majiji/ Halmashauri za Mji lakini yana sura ya vijiji ambayo wananchi wake wanalipa zaidi ya shilingi 27,000 kuunganisha umeme ili kuvitambua vijiji hivyo na kuja na mradi utakaohakikisha wananchi katika vijiji hivyo wanaunganishiwa umeme kwa shilingi 27,000 tu ndani ya mwaka mmoja.

” Serikali hii ya Dk. Samia Suluhu Hassan ni sikivu na haiwezi kuweka matabaka ya wananchi, mtu amekaa ng’ambo moja analipa 27,000 na ng’ambo nyingine analipa 320,000 hili halikubaliki, Serikali imesikia changamoto hii na inaifanyia kazi, tutahakikisha umeme unawaka katika vijiji ambavyo vipo ndani ya miji.” Alisema  Ndejembi

Kuhusu suala la kufikisha umeme kwenye Taasisi kama vile shule na zahanati aliitaka REA kufanya tathmini ili kutambua taasisi ambazo hazijapelekewa umeme katika vijiji vyenye umeme ili ziweze kuunganishiwa.

Aidha, kuhusu suala la mafuta alisema kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz kunaleta changamoto kubwa ya upatikanaji mafuta duniani kwani asilimia 20 ya nishati ya mafuta inatoka katika mlango bahari huo lakini kutokana na Serikali ya Tanzania kujali wananchi wake, nchi ina mafuta ya kutosha na hakuna kituo ambacho kimefungwa kwa kukosa nishati hiyo tofauti na baadhi ya maeneo mengine duniani.

Vilevile kuhusu bei ya mafuta alieleza kuwa Serikali inafanya kila jitihada ili ziwe himilivu huku ikihakikisha mafuta yanapatikana muda wote na hifadhi mpya ya mafuta inayojengwa jijini Dar es Salaam eneo la Kigamboni ikitoa hakikisho la uhifadhi wa mafuta.

Habari Zifananazo

6 Comments

  1. IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU

    WANAUME 490

    WANAWAKE 28

    JUMLA 518

  2. IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU - KATI HAO 10 WANAJUA HOTELI ZILIPO says:

    IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU

    WANAUME 490

    WANAWAKE 28

    JUMLA 518

  3. IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU - KATI HAO 70 WANAJUA LODGE ZILIPO says:

    IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU

    WANAUME 490

    WANAWAKE 28

    JUMLA 518

  4. IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU - KATI HAO 428 HAWAJUI HOTEL/LODGE ZILIPO says:

    IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU

    WANAUME 490

    WANAWAKE 28

    JUMLA 518

  5. IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU - KATI HAO 10 WANAJUA GUEST HOUSE ZILIPO says:

    IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU

    WANAUME 490

    WANAWAKE 28

    JUMLA 518

  6. IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU - KATI HAO 10 WANAJUA GUEST HOUSE ZILIPO. says:

    IDADI YA WATU WANAOFIKIRIA NYEGE KWENYE JIJI LA UTAKATIFU

    WANAUME 490

    WANAWAKE 28

    JUMLA 518

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button