Balozi awatoa hofu Watanzania treni SGR

Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Togolani Mavura amewatoa hofu wananchi juu ya maendeleo ya utengenezaji seti 10 za treni za kisasa na vichwa 17 vya treni vya umeme vitakavyotumika katika reli ya kisasa SGR nchini.

Balozi Mavura ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha kampuni ya Hyundai Rotem na kukagua maendeleo ya utengenezaji wa vifaa hivyo mjini changwon, korea ya kusini siku ya leo Julai 25, 2023 na kuonesha kuridhishwa na kazi iliyofanywa na kampuni hiyo mpaka sasa.

Aidha amesema biashara kati ya Tanznia na Korea ya kusini imeimarika zaidi kutokana na makampuni ya nchi hiyo kuhusika katika shughuli za ujenzi wa reli na utengenezaji wa vifaa vya uendeshaji wa reli ya kisasa.

Kwa upande wake meneja mradi wa ununuzi wa vifaa hivyo kutoka Shirika la Reli Tanzania, (TRC) mhandisi Kelvin Kimario ametoa ufafanuzi kuhusu utofauti wa vichwa vya treni vya umeme na seti za treni za kisasa EMU.

Wakati vichwa viwili vya treni vya umeme vikitegemewa kuingia nchini hivi karibuni kutoka Ujerumani, kampuni ya Hyundai Rotem inatarajia kuanza majaribio ya kiwandani ya seti za treni za kisasa mwishoni mwa mwaka huu.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button