Minada kichocheo wakulima wa kahawa

KAGERA: Wadau wa kahawa mkoani Kagera kupitia kikao cha wadau wa zao hilo wamepongeza mabadiliko ya kimfumo ya ununuzi kwa njia ya mnada na kudai kuwa mfumo huo umeongeza uwazi wa bei na ushawishi wa kulima kwa wingi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Yahya Kido amesema Mkoa wa Kagera unaendelea kufanya vizuri katika uzalishaji wa zao la kahawa, huku akibainisha kuwa hadi sasa mkoa huo unavuna kahawa zaidi ya tani 55 kutokana na wananchi wengi kufufua mashamba huku kiwango cha uzalishaji kilitarajiwa kuongezeka.

Akifungua mkutano wa wadau wa kahawa mkoani Kagera, Kido amesema kuwa Serikali kupitia ushirikiano na wadau mbalimbali imeendelea kusambaza miche ya kahawa kwa wananchi, huku kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita yaani kuanzia mwaka 2022 hadi 2025 miche milioni 36.75 tayari imetolewa kwa wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo muhimu la biashara.
Amesema katika msimu wa 2025/2026 pekee, miche milioni 13.7 ilisambazwa kwa wakulima kupitia ushirikiano kati ya Bodi ya Kahawa Tanzania, halmashauri, vikundi vya wakulima pamoja na sekta binafsi huku uwazi Wa kuwepoe kwa mnada na bei kupanda kutoka Sh 1,200 hadi kufikia Sh 4,000 na kuendelea kumeongeza chachu kwa familia kulima kwa wingi zao hilo.

Amesema kwa mwaka 2025/2026 zao la kahawa liliingiza Sh bilioni 28.8 fedha ambazo zilienda kwa wakulima na baadhi ya fedha zilienda halmashauri kama mapato ya ndani na kusaidia miradi ya wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa Tanzania, TCB Primus Kimaryo amesema bado kuna haja kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na wafanyabiashara wa zao hilo ili kudhibiti biashara ya kahawa inayofanyika kwa njia za magendo.

Amesema baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu wanatoka ndani ya jamii husika, hali inayochangia upotevu wa mapato kwa wakulima pamoja na Taifa kwa ujumla huku akidai kuwa bodi hiyo kama msimamizi Mkuu wa kahawa inashindwa kupata takwimu sahihi ikiwa baadhi ya kahawa hainunulik kwa njia ya mnada au kupitia vyama vya ushirika
Amesema serikali imetoa uwazi na sehemu sawa Kwa wafanyabiashara kushiriki minada moja kwa moja na kuchuana na bei zilizoko dunian na kudai kuwa kununua kahawa kwa kujificha ficha kwenye mashamba ya wakulima ni kudhoofisha juhudi za serikali zilizowekwa



