Balozi Kombo atakuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 27 ya CFR

DAR-ES-SALAAM : WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 27 ya Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR)

Mahafali hayo yatafanyika kesho Disemba 13, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 893 watatunukiwa tuzo za Astashahada, Stashahada, Shahada, Stashahada za Uzamili na Shahada ya Uzamili.Uongozi wa Kituo unawakaribisha katika mahafali hayo” imesema taarifa hiyo.

Advertisement

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt Salim Ahmed Salim kipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. SOMA: Wahitimu Dk Salim Ahmed Salim washauriwa kujiajiri

Pamoja na mambo mengine Kituo kina majukumu ya kutoa mafunzo, kufanya utafiti na kutoa huduma ya ushauri elekezi katika masuala ya diplomasia, uhusiano wa kimataifa, stratejia, usuluhishi wa migogoro na ujenzi wa amani.