BAADA ya muda mchache uliopita Yanga kutoa taarifa ya kuagana na Bangala, hatimaye Azam FC imemtambulisha rasmi mchezaji huyo na kusaini mkataba wa miaka miwili.
“Tumefikia makubaliano na klabu ya Yanga ya kumnunua, mchezaji kiraka, Yannick Bangala na amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Bangala karibu Mbagala.” Imeeleza taarifa ya Azam FC.
Awali, Yanga ilitoa taarifa ya kufikia makubaliano na klabu hiyo juu ya kumnunua mchezajji huyo raia wa DR Congo.
Bangala anakuwa mchezaji wa pili msimu huu kutoka Yanga kwenda Chamazi, baada ya Feisal Salum kufanya hivyo.