Barabara Biharamulo yazinduliwa rasmi

MRADI wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilometa 0.75 wenye thamani ya Sh milioni 423 unaolenga kuboresha mazingira na kukuza uchumi katika mji mdogo wa Biharamulo mkoani Kagera umezinduliwa leo.

Akizindua kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Godfrey Eliakimu Mnzava amewapongeza Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kwa kutekeleza mradi kwa viwango vya kisasa ambapo amewataka wanachi kuhakikisha wanatumia mradi wa barabara kukuza biashara zao kiuchumi .

Amesema utekelezaji wa barabara hiyo umeboresha mazingira ya mji na kufanya mji kuwa safi , na kuongeza kasi ya wananchi kutumia fursa zaidi katika kuingiza mazao kwani hakutakuwa na changamoto ya kukwama kwa usafiri.

Advertisement

“Nawapongeza TARURA kama msimamizi mkuu wa mradi huu wa kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana vyema kupitia mradi uliotekelezwa, serikali inaendelea kuweka mazingira safi kwa wanachi wanaoishi mjini na vijijini,natoa wito kwa wanachi kuhakikisha wanatumia kuwepo wa mradi huu kufanya biashara zao kwa masaa 24, kuongeza maduka ya kibiashara pembezoni mwa barabara na kusafirisha mazao yao kwa urahisi kutoka vijijini kuja mjini kwa sababu Hapa hawatakwama Tena kwa usafiri ,”amesema Mnzamva.

Meneja wa Tarura Wilaya ya Biharamulo, Masuka Lung’wecha amesema mradi huo umetekelezwa kwa kipindi cha miezi sita tangu Oktoba 2023 hadi April 2024 kutoka kwenye fedha za mfuko wa jimbo na baada ya mradi huo kukamilika wananchi wameanza kunufaika na wanaendelea na kufanyabiashara zao kwa saa 24.

Baadhi ya wanachi ambao wanatumia barabara hiyo akiwemo Alstedes Raphael amesema kuwa barabara hiyo ilikuwa inajaa maji na wananchi waliteseka na mafuriko kwa kipindi cha nyuma hivyo upepo wa barabara kubwa ni Fursa kubwa za kuinua uchumi wao kupitia biashara wanazoendelea kufanya .

/* */