Barabara ya Himo Njia Panda – Moshi – KIA Njia Panda yafungwa

WATUMIAJI wa Barabara Kuu ya Himo Njia Panda – Moshi – KIA Njia Panda wanataarifiwa kwamba kumetokea uharibifu wa barabara katika eneo lililopita bomba kubwa la maji safi karibu na mzunguko wa Arusha (Arusha Roundabout).
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Meneja wa Wakala ya Barabara Mkoa wa Kilimanjaro Machi 28, imeeleza kuwa kufuatia hali hiyo barabara hiyo imefungwa kupisha matengenezo.
“Watumiaji wa barabara kwa magari makubwa ya mizigo zaidi ya tani 10 mnashauriwa kutumia barabara mbadala ya Lucy Lameck – Ghala – Viwanda – Manyema – Mafuta -Nyerere – Bonite – Khambaita,”
“Watumiaji wa barabara kwa magari madogo wanaweza pia kutumia barabara ya YMCA – Kilimanjaro kupitia Bustani Alle,” imeeleza taarifa hiyo.



