Baraza la Mawaziri (SCTIFI) wakutana Kenya

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imeshiriki Mkutano wa 47 wa Baraza la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki (SCTIFI) na Mkutano wa Dharura Pili wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 25 Novemba 2025 jijini Nairobi, Kenya.
Mikutano hiyo pamoja na masuala mengine imepokea na kujadili taarifa za kamati zinazosimamia masuala ya Biashara, forodha, uwekezaji, kamati ya viwango na mamlaka ya ushindani ya Afrika Mashariki. SOMA: Makamu wa Rais Ashiriki Mkutano wa AU-EU Angola

Vilevile, mawaziri hao wamepokea na kujadili na orodha ya ada, tozo na ushuru usiozingatia usawa, unaotozwa na nchi wanachama kinyume na matakwa ya Ibara ya 10 na ya 15 ya Itifaki ya Umoja wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mikutano hiyo miwili muhimu umejumuisha Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango – Zanzibar, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango- Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil.Mkutano huo umehudhuriwa na nchi zote nane (8) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.





JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com